Watafiti katika taasisi ya Pasteur mjini Paris Ufaransa, wamekuwa wakichunguza mamia za sampuli za damu kujaribu kubuni mbinu za kupambana na virusi hivyo.
Kwa sasa wanajaribu kubaini ikiwa kujibaidili kwa umbo virusi hivyo, kutasababisha maambukizi zaidi na ikiwa wanaweza kufanya lolote kuhusu ambavyo ugonwja huo unapimwa mwilini na pia ambavyo madawa yanatumika mwilini kupambana na ugonjwa huo.
Pia wanataka kuchunguza na kufanyia utafiiti chanjo dhidi ya ugonjwa huo.
Ugonjwa wa Ebola umewaua watu ziadi ya elfu nane huko magharibi mwa Afrika, wengi kutoka Guinea , Sierra Leone na Liberia
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni