Rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim ametaadharisha amesema kuwa ni hatari kwa kuwa dunia haijajiandaa kupambana na ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi. |
Akiongea mjini Washington,Kim,amesema ni muhimu kwa Serikali, mashirika, Mashirika ya misaada na makampuni ya Bima kufanya kazi pamoja kujiandaa kukabiliana na maradhi hayo siku za usoni.
Zaidi ya Watu 8,500 wamepoteza maisha hasa nchini sierra leone, Guinea na Liberia.
Kim amesema Ebola imekuwa tishio ikizingatiwa idadi ya Watu waliopoteza maisha na kuathiri uchumi hivyo amesema jitihada zifanyike kuutokomeza kabisha ugonjwa wa Ebola na kuitaka dunia kujifunza kutokana na athari za ugonjwa huu kwa kuwa dunia itakabiliwa na maradhi mengine miaka ijayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni