Wakina mama, Tabu Mohamed na Mwajuma Chota ( katikati ) wakisutana kwa kuibiana mabwana.
Awali ilifahamika kwamba wanawake hao walikuwa wakiishi pamoja maeneo ya Kikundi, Kata ya Sultan Area mkoani hapa. Kwa mujibu wa madai ya mashuhuda waliokuwa wamefunga mtaa huo, Tabu ndiye aliyeanza ‘kuchepuka’ na kigogo huyo ambaye ni mume wa mtu aliyemnunulia gari aina ya Toyota Opa.
Madai yaliendelea kushushwa kwamba, Mwajuma ambaye ni mke wa mtu alipoona mwenzake anakula vinono, naye akajiweka.
Bendi ilikodiwa na Tabu Mohamed ili kumsuta shosti yake Mwajuma Chota.
Habari za mtaani zilidai kuwa katika
kujiweka, alifanikiwa kulamba mshiko wa shilingi elfu 80 kabla ya
kushtukiwa na Tabu huku naye akitaka kuhongwa gari kama mwenzake.
Ilielezwa kwamba katika kufuatilia, Tabu aligundua kuwa Mwajuma anachepuka na ‘mshefa’ wake ndipo akapanga mashambulizi ya vita vya ardhini.
Ilielezwa kwamba katika kufuatilia, Tabu aligundua kuwa Mwajuma anachepuka na ‘mshefa’ wake ndipo akapanga mashambulizi ya vita vya ardhini.
Kwa hasira, Tabu alishonesha sare za
‘madila’ na kununua mizinga ya pombe kali ambapo alienda kukodi
matarumbeta na watu wa kusuta.
Wakubwa kwa watoto wakishuhudia vimbwanga vya wakinamama hao.
Ilisemekana kwamba kabla ya tukio, watu walipiga pombe kisha wakamfuata nyumbani kwao, Mtaa wa Karume na kulianzisha.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda ambalo
liliwasili eneo la tukio ndani ya dakika sifuri juu ya tukio hilo,
Mwajuma alifunguka: “Namshangaa Tabu kuja kunifanyia vurugu wakati na
yeye ni mwizi tu. Huyo bwana ni mume wa mtu.”
Kwa upande wake, Tabu alidai Mwajuma ni shosti yake lakini alimtendea kitendo kibaya cha kutembea na bwana’ke.
Kwa upande wake, Tabu alidai Mwajuma ni shosti yake lakini alimtendea kitendo kibaya cha kutembea na bwana’ke.
Mmoja wa wamama hao, Tabu Mohamed akichukuliwa na polisi kwa kumletea fujo mwenzake, Mwajuma Chota.
Makamanda wa Polisi wakiimarisha ulinzi eneo la tukio.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni