Maharusi wakiwa na nyuso za furaha |
Viongozi wa juu nchini Misri wametoa tamko baada ya uvamizi wakati wa usiku katika nyumba inayotumiwa na wapenziu wa jinsia moja kukoga kwa pamoja mjini Cairo
Wanaume nane walikamatwa na sasa wanakabiliwa na kosa la kufanyia mzaha dini kosa ambalo limekuwa likituhumiwa watu wanaokamatwa kwa kushukiwa kujihusisha na vitendo vya wapenzi wa jinsia moja.
Mahaba ya jinsia moja hayajapigwa marufuku nchini Misri,lakini watu wanaoshukiwa kuwa si 'rizki' huweza kukabiliwa na mashtaka ya mzaha katika dini na ufisadi.
Wanaume hao nane walitiwa korokoroni siku za karibuni kwa kukiuka maadili ya umma na hii ni baada ya video moja kuachiliwa ikionyesha ndoa iliyofungwa ya wapenzi wa jinsia moja na kuanikwa katika mitandao ya kijamii.
Wanaume hao wanakabiliwa na tisho la kufungwa jela. Misako ya polisi dhidi ya vituo vinavyotumiwa na wapenzi wa jinsia moja imeongezeka sana katika siku za hivi karibuni nchini Misri.
Wanaume wanaokamatwa huenda wakafungwa jela ikiwa watapatikana na hatia.
Miongoni mwa waliokamatwa ni mmiliki wa nyumba ambako msako ulifanyika.
Anatuhumiwa kwa kugeuza nyumba hiyo kuwa kituo cha mafunzo ya vitendo vya kupotosha na vinavyokwenda kinyume na maadili.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu, yamelaani ambavyo Misri inawatendea wapenzi wa jinsia moja hasa kwa kuwafanyia uchunguzi kwa sehemu zao nyeti kubaini ikiwa wanashiriki mapenzi ya jinsia moja au la.
Tukio kubwa zaidi ambapo Misri iliwakamata washiriki wa mapznei ya jinsia moja ilikua mnamo mwaka 2001 wakati ambapo wanaume 52 walikamatwa katika ukumbi wa densi mjini Cairo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni