Mtu mmoja aliyejulikana
kwa jina la Peter sebastiani amejikuta akiwa katika maumivu makali baada ya
kumwagiwa kemilaki inayodaiwa kuwa ni tindikali pamoja na kuibiwa fedha
alizokuwepo nazo mfukoni na watu wasiojulikana
Tukio hili
limetokea juzi jumapili katika mtaa wa wambura wilayani maswa mkoani simiyu
baada ya bw.peter akiwa katika matembezi yake muda wa saa nne usiku gafla
alivamiwa na watu na kisha kumumwagia kemikali hiyo
Tatizo kubwa likidaiwa ni
kutokana na masuala ya siasa hasa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi huu
mnamo tarehe 14 kote nchini ambao ni uchaguzi wa ngazi ya vitongoji pamoja na
vijiji.Pia inadaiwa kuwa tatizo hili limetokea kutokana na vyama viwili ambavyo
ni chama cha demokrasia na maendeleo [CHADEMA] Pamoja na chama cha mapinduzi
[CCM]
Hadi sasa bw.peter
anaendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya ya maswa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni