Marehemu Alfred Ghozi enzi za uhai wake.
|
Mama wa marehemu Alfred Ghozi (26) akihuzunika kumpoteza mwanaye.
Tukio hilo la kutisha lilijiri mwanzoni mwa mwezi huu, katika
Kitongoji cha Kyawazaru Kata ya Kukirango wilayani Butiama, Mara.Licha
ya kuchinjwa shingo, mwili wa marehemu huyo ulikutwa na majeraha kibao
ikiwemo tumbo lake kupasuliwa na macho kutobolewa kwa kitu chenye ncha
kali.
WACHINJAJI AKINA NANI?
Chanzo cha habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara zinasema, mwalimu huyo alichinjwa kikatili na watu wasiojulikana lakini awali alipigiwa simu na mwanafunzi wake mmoja wa kidato cha nne (jina tunalihifadhi kwa sasa), mwenye umri wa miaka 23 ambaye alitoweka na anatafutwa.

DAKIKA ZA MWISHO ZA UHAI WAKE Taarifa
zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, ACP Alex
Kalangi zinaelezea kwa kina jinsi mwalimu huyo alivyopita katika dakika
za mwisho za uhai wake wa duniani.
Waombolezaji wakimfariji mama wa marehemu Alfred Ghozi msibani.
Inadaiwa Desemba 7, mwaka huu, saa 1:30, marehemu aliondoka Kiabakari
akiaga kwa watu wake wa karibu kwamba anakwenda kwenye Mgodi wa Dhahabu
wa Kataryo uliopo kata hiyo baada ya kupigiwa simu na mwanafunzi huyo
aliyekuwa akimdai shilingi 450,000.
“Kwa mujibu wa vyanzo vyetu ni kwamba mwanafunzi huyo alimpigia simu
mwalimu wake aende mgodini ili akamlipe fedha alizokuwa akimdai.“Mwalimu
huyo kwa vile alikuwa na safari ya kwenda kwao, Kagera kwa likizo ya
Desemba aliamua kuzifuata fedha hizo kama alivyaombiwa na mwanafunzi
wake,” kilisema chanzo ndani ya jeshi la polisi.
MWALIMU AENDA KIMOJA
Habari zaidi zinasema, mara baada ya Mwalimu Ghozi kwenda kuitikia wito wa mwanafunzi wake ambaye pia anajishughulisha na uchimbaji wa dhahabu kipindi hiki cha likizo, hakurejea tena nyumbani kwake.
Ilipofika Desemba 9, mwaka huu, baadhi ya watu wake wa karibu walianza kujiuliza kisa cha mwalimu huyo kutorejea kwake lakini halikupatikana jibu la wazi.

Ndugu na jamaa wa karibu wakitoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Alfred Ghozi.
Wapo waliokataa kuamini kwamba huenda alikutana na mkasa mzito njiani
akienda au akirejea kwa vile mwalimu huyo hakuwa na tabia ya
kumuwezesha kuwa na maadui.
WANANCHI WAKUSANYIKA
Baada ya kuona hali si ya kawaida, baadhi ya wananchi, wakiwemo bodaboda wa Kiabakari, walikusanyika wakiongozwa na wapanda pikipiki wa Kiabakari na kuelekea mgodini ambako mwalimu huyo aliaga anakwenda kufuata fedha zake.

Lakini wakiwa wanakaribia mgodini, walimkuta mwalimu huyo kichakani
akiwa umechinjwa shingo, mwili wake umekatwakatwa sehemu mbalimbali hasa
tumboni kiasi cha kuufanya utumbo kuwa nje.
MWANAFUNZI ATOROKA
Akiongoza waombolezaji katika shughuli ya kuuaga mwili wa mwalimu huyo, Desemba 10, mwaka huu katika Viwanja vya Shule Sekondari ya Kukirango, Mkuu wa Wilaya ya Bitiama, Angela Mabula alilaani mauaji hayo ya kinyama.

Mabula akawataka wananchi kushirikiana na polisi kuwajua watu
waliomchinja mwalimu huyo, akiwemo mwanafunzi huyo ambaye inaaminika
alitumika kumuita marehemu kwa kumlaghai kuwa anataka kumlipa deni lake
kumbe sivyo.
“Wahusika wote wa mauaji hayo akiwemo mwanafunzi wametoroka, hivyo
kuwapa kazi polisi kuwasaka na kuwakamata ili wawafikishe kwenye vyombo
vya sheria, mshirikiane nao,” alisema mkuu huyo wa wilaya.
Kamanda Kalangi aliyekiri kutokea tukio hilo, alisema hajakamatwa mtu
yeyote kuhusiana na mauaji hayo lakini makachero wa polisi bado wapo
kazini wakiendelea na msako.
Marehemu alizikwa Mjini Bukoba, Kagera mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.
Marehemu alizikwa Mjini Bukoba, Kagera mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni