Blass Band ya Jeshi la Polisi ikiongoza maandamano ya Maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani na Miaka 66 ya Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu. Maandamano hayo yaliyoanzia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima hadi Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam leo asubuhi yaliandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC). |
Maandamano yakiendelea barabara ya Ohio.
Maandamano yakiingia Makumbusho ya Taifa barabara ya Shabani Robert.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Ezekiel
Masanja akitoa hutuba katika maadhimisho hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa
Bodi ya LHRC, Profesa Geofrey Mmari.
Wawakirishi wa mashirika mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mwanasheria wa LHRC, Halord Sungusia akitoa mada katika maadhimisho hayo.
Wanakwaya wa Kwaya cha Mwalusanya ambao wapo chini ya LHRC wakitoa burudani za nyimbo za uhamasishaji.
Wadau mbalimbali na wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Wadau mbalimbali na wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesema kiwango cha
elimu ya haki za binadamu nchini bado kipo chini hali inayosababisha
kukithiri kwa makundi ya ukatili wa kinjia nchini.
Kufuatia hali hiyo kituo hicho kinaishauri Serikali kujumuisha
elimu ya haki za binadamu kwenye mfumo wa elimu rasmi inayotolewa nchini
ili kupanua uelewa kwa jamii.
Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo na Kaimu Mkurungezi Mtendaji wa
kituo hicho, Ezekiel Masanja wakati wa hitimisho la siku kumi na sita za
kupinga ukatili wa kijinsia duniani.
Akitoa takwimu za nusu mwaka dhidi ya vitendo vya ukatili wa jinsia
Masanja alisema wanawake na wasichana 2878 walibakwa, vilvile vitendo
vilivyoripotiwa polisi nchi nzima ni 3,633.
''Ukatili upo katika makundi mbalimbali kama vile mauaji ya
vikongwe, albino watoto kubakwa lakini, ukatili, unyanyasaji ambao mara
nyingi unafanywa na ndugu jamaa wa karibu ambao sio rahisi kuwatambua
kwa haraka,'' alisema.
Aliongeza kuwa kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi iliyofanyika
mwaka 2012 idadi ya watanzania waliopata elimu rasmi ni zaidi ya milioni
14 kati yao watu ni zaidi ya milioni 11 wamehitimu elimu ya msigi,
wenye elimu ya chuo kikuu ni zaidi ya laki tatu 3.3.
"Hali hii inabainisha watu walio na elimu ya dhidi ya haki za
binadamu ni wachache ukilinganisha na mahitaji changamoto inayotokana na
mifumo ya elimu rasmi inayotolewa nchini ,"alisema.
Akizungumzia kura ya maoni inayotarajiwa kupigwa mwakani alisema
wananchi bado hawana uelewa wa kutosha dhidi ya katiba inayopendekezwa.
"Naiomba Serikali kutoa mwamko kwa wananchi kwa kusambaza kopi
nyingi za rasimu inayopendekezwa kusudi kuwasaidia wananchi kuelewa nini
wanaenda kupigia kura , "alisema. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni