Mganga wa tiba za asili Omar Kikukwa mwenye miaka 32 Wilayani Kilindi
anashikiliwa na polisi kwa kuwachoma moto wateja wake na kusababisha
mmoja wao kufariki dunia.
Aziza Hassan mmoja wa wnaafamilia walionusurika katika mkasa huo
alisema mama yake pamoja na watoto wake wawili walipelekwa kwa mganga wa
kienyeji na baba yao wa kufikia kwa ajili ya kufanyiwa tambiko.
Alisema kuwa walipofika kwa mganga huyo na kuanza kufanyiwa dawa
ambapo ilifanyika ndani ya shimo ambalo liliezekwa kwa nyasi juu yake na
kuachwa nafasi ndogo kwa ajili ya kuingilia ndani ya shimo waliloambiwa
ndipo dawa inatakiwa kufanyika huku baba yao akibaki nje na mganga.
Alisema baada ya muda walidhani mganga ameshamaliza na aliwajibu
dawa bado inaendelea na gafla mganga huyo aliwasha moto mkubwa na kuanza
kuwaka ndipo akawaamrisha watoke shimoni huku moto ukiendelea kuwaka
hadi mlangoni.
Alisema baada ya moto kupungua walitoka huku wenzake wakiwa
hawajiwezi kabisaambapo baba yakena mganga waliwakataza kwenda hospitali
na kuwaambia kuna daktari wao anakwenda kuwatibu katika kijiji cha
jirani na hapo huku mwenzao mmoja akipoteza maisha.
Kwa sasa mganga huyo anashikiliwa na polisi kwa kosa lakusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wengine watatu kwa moto.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni