Bi Lawaridi Said |
Katika
hali isiyo kuwa ya kawaida mama moja aliye kuwa akisafiri na mtoto
wake mmoja na wajukuu zake wawili, aliamua kumtupa mjukuu wake wa miaka
sita dirishani huku basi likiwa katika mwendo kasi na kusababisha kifo
chake baada ya kufikishwa katika hospitali ya mkoa wa Singida.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida ACP
Thobias Sedoyeka, amesema mama huyo aliye tambulika kwa jina la Lawaridi
Saidi mweye umri wa miaka 46 aliyekuwa akisafiri na basi namba T 981
ALS kampuni ya Salumu Clasc lilokuwa likitokea Dar-es-salaam na kuelekea
Kigoma.
Amesema
alipofika katika kijiji cha Iguguno wilaya ya Mkalama siku ya tarehe
18/12/2014 saa 2 usiku alimtupa mjukuu wake Mayasa Meshack dirisani huku
basi likiwa katika mwendo kasi.
Tayari jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia mwanamke huyo.
Tayari jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia mwanamke huyo.
Mganga
wa zamu katika Hospitali ya Mkoa wa Singida Dkt Adamu Hussen amesema
alimpoke mtoto akiwa katika hali mbaya akiwa hapumui vizuri na damu
ilikuwa ikimtoka masikioni na baada ya kumpatia matibabu alilazwa na
siku ya pili alifariki dunia kutokana na kupasuka kwa fuvu la kichwa.
Akieleza
jinsi alivyo mtupa mjukuu waka,Lawaridi Saidi ambaye ni mkazi wa K
ongowe jijini Dar es salaam amesema baada ya kuamka akiwa katika hali
ya usingizi alijikuta akimchukua mjukuu wake Mayasa na kumtupa
dirishani na hatimaye abiria wakaanza kumpiga na kuamuru basi lisimame
na kumchukua mtoto huyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni