Mkurugenzi wa TCRA, Prof. John Nkoma |
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetoa mwongozo kwa wamiliki wa mitandao ya kijamii (Bloggers), ili kutoa taarifa zenye usahihi hususani kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwakani.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaan na Mkurugenzi wa TCRA, Prof. John Nkoma, (pichani) katika mkutano uliowakutanisha mamlaka hiyo na wamiliki hao.
“Blogs ni wadau wetu, tunafahamu kuwa Blogs zinatumiwa na watu wengi sana katika kupashana habari, hivyo kuna haja ya kuelimisha, kutahadharisha, kuhakiki na kuwa ‘accuracy’ (usahihi) na kubalance habari bila kupendelea mtu na kumkashifu, na kumpa mtu nafasi ya kujieleza,” alisema Prof. Nkoma.
Aidha, alisisitiza kuwapo kwa kanuni, mipaka na taratibu katika masuala ya habari na kwamba uhuru unaishia katika mipaka.
Naye Mmiliki wa Blog ya Matukio Daima, Francis Godwin, alisema katika kuelekea uchaguzi mkuu mwakani, wataunda chama chao kitakachoweza kutoa mwongozo na kuweka kanuni zao.

“Kuna changamoto kubwa, wamiliki wa Blogs baadhi hawana elimu ya mawasiliano na habari, lakini mmiliki kama si yeye kujiendeleza anaweza kuwatumia wataalamu wa fani hii, chama kitasaidia kuwajibishana wenyewe,” alisema Godwin.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni