Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akionyesha stika alizokabidhiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia |
Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Bararani, linatarajia
kuanzisha operesheni ya lazima ya kukagua magari ili kukabiliana na
ajali za mara kwa mara.
Hayo yalisemwa na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga (pichani), jijini Dar es Salaam jana.
Kamanda Mpinga alifafanua kuwa operesheni hiyo itawahusu madereva wa magari aina zote.
“Lengo kuu la operesheni hii ni kukabiliana na ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara na kusababisha watu kupoteza maisha yao kutokana na madereva wengi kutofuata kanuni na taratibu za usalama barabarani,” alisema Kamanda Mpinga.
Aidha, alisema ukaguzi huo utakaotumia mitambo maalum, utalenga zaidi kwenye mambo muhimu ambayo ni pamoja na leseni, stika maalum za magari, mfumo wa breki, mwendo kasi, injini, matairi, usukani na mfumo wa umeme.
“Operesheni hii itafanywa kwa umakini zaidi na wataalam wote wa usalama barabarani na tunaamini itapunguza ongezeko la ajali za barabarani kwa kiwango kikubwa sana,” alisema Kamanda Mpinga.
Aidha, alisema pia wataanzisha program ya kuwafanyia majaribio madereva waliofaulu mafunzo ya udereva na kupata leseni ili kubaini kama walifuata taratibu na kanuni zote kutokana na udanganyifu mwingi kutumika, hali ambayo huchangia ajali za barabarani kutopungua.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni