Hot news kutoka Coventry, Uingereza inamhusu Ayan Qureshi ambaye ana umri wa miaka sita tu, na mwaka jana aliingia kwenye list ya watoto waliofanya maajabu ambapo alifanya mtihani wa kampuni ya Microsoft unaothibitisha wataalamu wa IT duniani na kufaulu.
Baba yake ambaye ni mtaalamu wa IT anasema alimfundisha mtoto wake kuhusu masuala ya Kompyuta tangu akiwa ana umri wa miaka mitatu.
Katika mahojiano na mtoto huyo amesema mtihani ulikuwa mgumu lakini alienjoy kuufanya na alijiandaa kwa miezi mingi kabla ya kuufanya, kutokana na kufaulu mtihani huo kwa sasa anakuwa ni mtaalamu wa IT aliyethibitishwa na Microsoft ambaye ana umri mdogo zaidi duniani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni