promotion

Jumatatu, 10 Novemba 2014

`Misamaha ya kodi siyo njia pekee kuhamasisha uwekezaji







Katibu Mkuu wa Mtandao wa Wabunge unaopambana na rushwa, (APNAC), Vita Kawawa (pichani), amesema misamaha ya kodi inayotolewa na serikali siyo njia pekee ya kuhamasisha uwekezaji nchini na alitaja  ametaja mambo mbadala, ambayo yakiboreshwa yatakuza uwekezaji bila serikali kutoa misamaha hiyo.


Kauli hiyo ya Kawawa iliungwa mkono na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, ambaye alisema misamaha hiyo mingi hutolewa kwa wawekezaji wakubwa, kama vile wanaowekeza kwenye mahoteli makubwa ya kifahari, migodi ya madini na gesi huku wawekezaji wadogo wengi wakiwa wananchi wakibanwa ili walipe kodi.


Kauli hizo zilitolewa jana kwenye semina iliyoandaliwa na kuendeshwa kwa ushirikiano wa Mtandao wa asasi za kiraia zaidi ya 900, zinazotetea haki na usawa kwa walipa kodi na APNAC kwa wabunge, ili kuboresha miswada miwili ya kodi itakayowasilishwa katika vikao vya bunge vinavyoendelea.


Miswada hiyo ni wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na wa Utawala wa Kodi. 

Alisema badala ya kuendelea kutoa misamaha ya kodi, ambayo imethibitika kuwa miongoni mwa vyanzo vikuu vya kukwamisha maendeleo ya taifa, serikali iboreshe miundombinu ya usafirishaji, huduma za maji, umeme upatikane kwa uhakika, urasimu ukomeshwe na rushwa ipunguzwe ikibidi imalizwe kabisa.


Ndugai alisema moja ya madhara yanayotokana na kasoro katika utoaji wa misamaha kwa walipa kodi nchini, ni bajeti ya taifa kutegemea misaada kutoka kwa wahisani.

Hakuna maoni: