Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI),Athuman Diwani. |
Watu saba wameuawa wilayani Kiteto, mkoani Manyara, baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya wakulima na wafugaji.
Mauaji hayo yalitokea tangu Novemba 11 na 15 baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya pande hizo mbili yaliyosababishwa na mgogoro wa ardhi.
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Athuman Diwani, alithibitisha kuuawa kwa watu hao.
Diwani aliwataja waliouawa kuwa ni Hassani Kundajo (62), Lematui Sendalo (46), Maria Olesiriana (36), Julius Adrea (50), Jobu Makavu (42), Juma Omari Bakari (65) na Salum Iddi Juma (70).
Aliongeza kuwa miili ya watu hao ilikutwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao ikiwamo kichwani, kifuani na miguuni, hali inayoonyesha waliuawa kwa kutumia silaha za jadi zenye ncha kali.
Alisema tayari Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa 13 kutokana na tukio hilo, huku uchunguzi ukiendelea.
Alitoa onyo kwa yeyote atakaebainika kuhusika katika vitendo hivyo atachukuliwa hatua kali bila kujali nafasi yake katika jamii.
Mgogoro huo wa ardhi kati ya wakulima na wafugaji ulianza mwaka 2003, kwa kugombania ardhi ya pori la Hifadhi ya Emborey Mutangozi lenye hekta 133.
Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo, alilaani kitendo hicho na kwamba hawako tayari kukivumilia.
“Kitendo hiki kilichofanywa ni cha kinyama ambacho hakivumiliki na mtu yeyote katika taifa lolote, ni lazima wahusika wachukuliwe hatua kali za kisheria,” alisema Mbwilo.
Aliongeza kwamba wao kama Kamati ya Ulinzi na Usalama watahakikisha wanashughulikia suala hilo na kurejesha hali ya amani kama ilivyokuwa awali.
Novemba 11 mwaka huu Naibu Spika na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai, alisema vitendo hivyo vya mauaji vimekuwa vikifanywa kana kwamba hakuna hatua zinazochukuliwa na serikali mkoani humo.
Ndugai alisema hayo bungeni wakati alipokuwa akijibu mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Moza Abeid, aliyetaka kufahamu hatua ambazo serikali imechukua kuhusiana na mgogoro huo.
“Kiteto ni kama haiko Tanzania. Ninyi (wabunge) leo mnasikia tu hamjui kitu gani kinachotokea huko, hali ni mbaya sana,” alisema Ndugai na kuongeza:

“Kinachozungumziwa ni mauaji na siyo mgogoro wa wakulima na wafugaji, watu wanauawa kana kwamba vinakofanyika vitendo hivyo siyo Tanzania, tatizo kubwa kule ni silaha ambazo zimezagaa.”
Akizungumzia hali hiyo mwishoni mwa wiki Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azan Zungu, alisema kamati iliazimia kwamba serikali kupitia Waziri Mkuu ingetoa maelezo kwa kamati hiyo Novemba 14 jioni juu ya jambo hilo, na kueleza namna lilivyoshughulikiwa kipindi cha nyuma, kisha itolewe taarifa kamili bungeni.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni