HABARI KAMILI
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, msala huo ulijiri juzikati nyumbani kwa ticha huyo, Kichangani ambapo mwalimu huyo alidaiwa kufumwa na mume wa mtu, Raphael Bernard (33) ambaye ni dereva wa bodaboda.
ILIKUWAJE?
Habari zilidai kwamba mwenye mume amekuwa akimfuatilia mumewe kwa muda mrefu, akagundua huwa anakwenda kujichimbia kwa ticha huyo huku akiacha familia ikilala njaa.
Ilisemekana kuwa, siku ya tukio, mwenye mume, akiwa na ‘jeshi’ lake, alimfuatilia mumewe hadi akamuona akiingia nyumbani kwa hawara wake huyo.
APEWA MUDA AVUTE PUMZI
Ikazidi kudaiwa kwamba baada ya kuhakikisha jamaa amelala kwa ticha huyo, mwanamke huyo na ‘skwadi’ yake waliondoka, asubuhi iliyofuata mishale ya saa 1:04 wakatia timu na kulianzisha timbwili huku mke huyo akidaiwa kumtishia ticha kuwa akipata ujauzito atazaa kwa mdomo.
Habari zinadai kuwa, baada ya mke huyo na timu yake kuondoka, ticha
huyo alimuwakia Raphael kwamba kumbe ana mke, kwa nini hakuwahi
kumwambia? Ugomvi mwingine ukazuka hapo.Ikazidi kudaiwa kwamba baada ya kuhakikisha jamaa amelala kwa ticha huyo, mwanamke huyo na ‘skwadi’ yake waliondoka, asubuhi iliyofuata mishale ya saa 1:04 wakatia timu na kulianzisha timbwili huku mke huyo akidaiwa kumtishia ticha kuwa akipata ujauzito atazaa kwa mdomo.
MASHUHUDA SASA
Nao mashuhuda ambao ni majirani wa mwalimu huyo, Juma Hamis na Joyce Joseph, walipozungumza na paparazi wetu walisema siku hiyo walisikia vurugu kutoka ndani kwa mwalimu ambapo walikwenda kushuhudia.
Walisema walimkuta mwanaume huyo akipigana na ticha ambaye alikuwa akiendelea kulalamika kufichwa suala la mwanaume wake kuwa na mke.
WACHOMANA VISU
“Unaambiwa mzozo huo ulipamba moto, maana yule mke aliyeondoka alidai amemfumania mumewe, mwalimu naye akadai alikuwa hajui.
“Katika purukushani hiyo huku wakipigana wao kwa wao ndipo wakachomana visu. Yaani mwanaume alijeruhiwa vibaya mno.
“Mwanaume alichomwa kisu utumbo ukatoka nje na kama siyo polisi
kufika na kukimbizwa hospitalini, sasa hivi tungekuwa tunaimba
‘Parapanda Italia….Parapanda…’ kwani hali ilikuwa mbaya sana,” alisema
Joyce kwa masikitiko.HOSPITALINI
Baada ya kuzungumza na majirani na mashuhuda wa tukio hilo, mwanahabari wetu alitia gia kwenye pikipiki yake aina ya ‘boksa’ hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Mwandishi wetu alizungumza na Kaimu Mganga Mfawidhi, Dk. Francis Semwene ambaye alikiri kuwapokea majeruhi hao.
“Mwanaume alikuwa amepasuka tumboni hivyo tunaendelea kumpa matibabu, yupo wodi namba moja na mwanamke ambaye naye amechomwa visu sehemu mbalimbali za mwili wake, naye tunaendelea kumpatia matibabu,” alisema Dk. Semwene.
HUYU HAPA MWANAUME
Akizungumza na mwanahabari wetu kwa tabu huku polisi wakiwa wamempiga pingu kitandani, Raphael alisimulia kwa maumivu makali:
“Mke wangu ni Veronica lbrahim ambaye tumeishi kwa miaka 6 na kujaliwa kupata mtoto mmoja.Akizungumza na mwanahabari wetu kwa tabu huku polisi wakiwa wamempiga pingu kitandani, Raphael alisimulia kwa maumivu makali:
“Mwezi wa tano mwaka huu, tuligombana, niliondoka nyumbani, kwa heshima ya mtoto wangu, sikuchukua kitu chochote zaidi ya nguo.
“Mwezi huohuo nilifanikiwa kuingia kwenye uhusiano na Mwalimu Rosemary ambapo baada ya penzi kukolea aliniambia nihamie kwake ili tulifaidi penzi letu tamu yaani mahaba motomoto na niliishi pale miezi mitano.”
FUMANIZI?
Alipotakiwa kuelezea chanzo cha tukio la fumanizi, jamaa alifunguka: “Hamna. Ticha aliniamsha asubuhi akaniambia nimsaidie kufanya usafi na kumuogesha mwanaye.
MADAWA YA KIENYEJI
“Nilipomaliza kumuogesha nilitaka kutandika kitanda, nilipoinua godoro niliona madawa ya kienyeji.
“Nilipomuuliza mwenzangu akawa mkali kama pilipili ndipo ugomvi mkubwa ukaanzia hapo.
“Baada ya mzozo mkali, ndugu zake walinivamia, akiwemo shemeji yangu wa kiume, namfahamu kwa jina la baba Dickson.
MAUMIVU
“Wakati najitetea, nilishika kisu ambapo katika hekaheka ya kunyang’anyana na Rosemary kilinichoma mimi na yeye.”
TICHA ARUHUSIWA
Mwandishi wetu alifika wodi namba tatu aliyolazwa ticha huyo na kuelezwa kuwa aliruhusiwa baada ya kupata nafuu ya majeraha mengi ya visu aliyoyapata sehemu mbalimbali za mwili wake hasa kichwani.
Baada ya kumkosa ticha huyo wodini, gazeti hili lilimfuata nyumbani kwake, alipobanwa alisema:
”Tukio hili limetokana na ushirikina wa mke wa zamani, alinitishia kuwa nikishika mimba nitajifungulia mdomoni akiapa kunifanyia kitu mbaya.
“Yaani hata sijui nini kimetokea, Raphael, mume wangu kipenzi amenichoma kisu na yeye kujichoma tumboni.”
KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Tukio hilo liliripotiwa Oktoba 27, mwaka huu, ambapo Raphael alikwenda kwa mpenzi wake, Rosemary ambako kulitokea ugomvi, wakaumizana kisa wivu wa kimapenzi, hivyo tunamshikilia mwanaume huyo huku uchunguzi ukiendelea,” alisema Kamanda Paul.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni