promotion

Alhamisi, 27 Novemba 2014

BABA WA MSANII ASHUSHA KICHAPO



Baba mmoja ambaye jina halikupatikana mara ameshusha kichapo kwa wasanii ambao ni maprodyuza waliokuwa wakimchezesha mwanaye filamu bila ridhaa yake.
Baba huyo akizuiwa ili asiendelee kushusha kichapo hicho.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, tukio hilo lilijiri juzikati, maeneo  ya Mwananyamala-Komakoma jijini Dar ambapo awali binti huyo ambaye ni msanii chipukizi wa kuigiza aitwaye Jeniffer alidaiwa kupigwa mkwara na baba yake kuwa asijishughulishe na masuala ya muvi na badala yake ajikite kwenye masomo yake kufuatia tasnia hiyo kuhusishwa na skendo za ngono.
Ilidaiwa kwamba, Jeniffer alikaidi amri ya mzee wake huyo na kwenda kinyemela kurekodi vipande kadhaa vya muvi ya kikundi chao ambapo taarifa zilimfikia baba yake huyo na kuamua kutimba lokesheni.
Baba huyo akijiandaa kumvaa prodyuza huyo.
Ilisemekana kwamba, katika hali iliyompandisha zaidi hasira, mzee huyo alipofika maeneo hayo alimkuta mwanaye katikati ya ‘scene’ ya mahaba aliyokuwa akiigiza na msanii anayetamba kwenye Tamthiliya ya Siri ya Mtungi, Daudi Michael almaarufu Duma.
Baada kushuhudia bintiye ‘akigaragazwa’ kimahaba, mzazi huyo alimvaa msanii Duma na kumshutumu kumharibia binti yake ambapo alimpa kibano pamoja na maprodyusza wenzake kabla ya kuamuliwa na wasanii wengine waliokuwepo eneo hilo.
Watu waliokwepo kwenye sakata hilo wakiamulizia.
Ilidaiwa kwamba, alipoona amewakungung’uta vya kutosha, baba huyo aliondoka na bintiye akiahidi kwenda ‘kumsulubu’ nyumbani kwa kuwa amekuwa sikio la kufa.
Kwa upande wake, Duma alibaki na majeraha mgongoni ambayo hadi waandishi wetu wanafika eneo la tukio yalikuwa yakitoka damu.
Duma alipoulizwa kuhusiana na mzee huyo, alikana kumfahamu na kudai kuwa alipewa mamlaka ya kumtumia binti huyo kwenye muvi na kaka wa msichana huyo.
Baba huyo akiondoka na binti yake.
“Nilimuomba Jeniffer kwa kaka yake na alikubali nishuti naye, sasa sijui nitafanyaje maana tulishashuti scene kibao halafu Jeniffer kashindwa kumalizia,” alisema Duma.


Imeandaliwa na Deogratius Mongela, Chande Abdallah na Denis Mtima.


Hakuna maoni: