“Tazama Ramani Utaona Nchi Nzuri” ni wimbo unaoelezea mali asili na vivutio vizuri vya utalii nchiniTanzania. Nchi yenye mito, maziwa na mabonde mazuri.
1. Tazama ramani utaona nchi nzur i
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka,
Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,
Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzania
2. Chemchem ya furaha amani nipe tumaini,
Kila mara niwe kwako nikiburudika,
Nakupenda sana hata nikakusitiri,
Nitalalamika kukuacha Tanzania.
3. Nchi yenye azimio lenye tumaini,
Ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania,
Ninakuthamini hadharani na moyoni,
Unilinde name nikulinde hata kufa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni