promotion

Jumanne, 21 Oktoba 2014

PISTORIOUS AFUNGWA MIAKA 5






















Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.
Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.
Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius akiwa na mpenzi wake Reeva Steenkamp enzi za uhai wake.
jaji aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa,alianza kutoa kauli yake ya mwisho kabla ya kutoa hukumu saa mbili na nusu asubuhi na akasema ni changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye kesi hiyo.
Jaji aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa.
Upande wa mashitaka ulitaka mwanariadha huyo kupewa kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kupatikana na makosa ya kuua bila kukusudia.
Pistorius alisema kuwa alifyatua risasi baada ya kudhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.
Upande wa mashitaka unasisitiza afungwe jela wakati wakili wa Pistorius wakimtaka jaji ampe kifgungo cha nyumbani cha miaka mitatu na pia apewe usaidizi na ushauri wa kubadili tabia yake.

Hakuna maoni: