Mlinda mlango wa klabu ya Orlando Pirates ya Afrika kusini Senzo Robert Meyiwa, amefikwa na umauti baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana mwishoni mwa juma lililopita.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na jeshi la piolisi nchini Afrika kusini Meyiwa alifikwa na mkasa wa kupigwa risasi baada ya watu wawili kumvamia katika nyumba aliyokuwa amepumzika maeneneo ya Valorous, nje kidogo ya jiji la Johannesburg.
Taarifa ya jeshi la Posili imeendelea kubainisha kwamba tukio hilo lilijitokeza mishael ya saa mbili usiku kwa saa za Afrika kusini ambapo imethibitika watu hao wawili walioingia ndani waliongozana na mtu mwingine ambae alibaki nje ya nyumba iliyoshuhudia tukio hilo.
Hata hivyo Meyiwa aliaga dunia baada ya kufikishwa hospitalini.
Jeshi la polisi nchini Afrika kusini limeahidi kufanya jitihada za kuwasaka wahalifu waliohusika na tukio la kifo cha mlinda mlango huyo alieaga dunia akiwa na umri wa miaka 27.
Siku ya jumamosi Meyiwa alikuwa sehemu ya kikosi cha Orlando Pirates wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la ligi huko Afrika kusini.
Pia mlinda mlango huyo atakumbukwa kwa mchango wake alioutoa kwenye michezo minne iliyopita ya timu ya taifa ya Afrika kusini ya kuwania kufuzu katika fainali za Afrika ambapo Meyiwa aliweza kuwa nahodha katika mipambano hiyo.
Kifo cha Meyiwa kimefuatana na kile cha aliyekuwa bingwa wa mbio za mita 800 Mbulaeni Mulaudzi, kilichotookea siku ya ijumaa huku tukio lingine ambalo bado linakumbukwa nchini Afrika kusini ni lile la kufungwa kwa mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius, aliyehukumiwa miaka mitano jela kufuatia kosa la kumuua bila kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Kwa mujibu wa jeshi la polisi nchini Afrika kusini, zaidi ya watu 17,000 nchini humo wameshahukumiwa kwa makosa ya mauaja ambapo matukio ya watu hao yamejitokeza kati ya mwezi April mwaka 2013 hadi mwezi March mwaka 2014, ikiwa ni ongezeko la watu 800 kwa kipindi cha miaka iliyopita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni