promotion

Ijumaa, 31 Oktoba 2014

Kiwango cha kalori katika pombe kitajwe




Pombe inatakiwa kuwa na nembo inayoonyesha kiwango cha kalori au kipimo cha joto litolewalo na chakula ili kupunguza vitambi au unene wa kupita kiasi.
Madaktari wa afya ya umma, wameonya kuwa glasi kubwa ya mvinyo inaweza kuwa na kiasi cha kalori 200- sawa na donati, aina ya maandazi.
Hata hivyo idadi kubwa ya watu hawajui madhara ya kula kiwango kikubwa cha kalori.
Waziri wa Afya Jane Ellison amesema "hatua kubwa" imefanyika kwa kuviwekea nembo vyakula, na kwa suala hilo serikali italiangalia.
Sekta ya vinywaji imesema imesema iko tayari kwa wazo hilo la kuweka nembo zenye kuonyesha kiasi cha kalori, lakini kuweka nembo zinazonyesha kiwango cha kilevi katika kinywaji ni muhimu zaidi.
Uingereza ni moja ya mataifa yenye watu wenye unene wa kupita kiasi duniani kwa kuwa na idadi ya karibu robo ya watu wazima kuwekwa katika kundi la wenye unene wa kupitiliza.
Vyakula tayari vinakuwa na taarifa za kiasi cha kalori kilichomo ndani yake, lakini pombe haimo katika sheria za Umoja wa Ulaya zinazotaka vyakula viwekewe nembo.
Mvinyo nao watakiwa kuonyesha kiwango cha kalori
Na Tume ya Ulaya inaangaliwa iwapo vinywaji viwekewe nembo yenye kuonyesha kiasi cha kalori kilichomo.
Utafiti uliofanywa na Chama cha Masuala ya Afya ya Jamii nchini Uingereza, umesema hatua hii itaungwa mkono na wanywaji nchini Uingereza.
Mkuu wa chama hicho cha RSPH, Shirley Cramer, ameiambia BBC: "Ni jambo la kushtusha kweli - asilimia 80% ya watu wazima hawana wazo la kujua kiasi cha kalori kilichomo katika kinywaji chochote na kama wanafikiri wana wazo hilo kwa ujumla wanakadiria kiasi cha chini mno."
"Itasaidia taifa kupunguza watu wenye unene wa kupitiliza na huenda kupunguza kupunguza unywaji wa pombe."

Kiasi cha kalori:

Glasi kubwa ya 250ml ya mvinyo wenye kileo cha asilimia 8% ni kalori 170 Kiasi hicho hicho cha glasi ya 250ml ya mvinyo wenye kileo cha asilimia 14% ni kalori 230 Painti moja yenye asilimia 4% ya bia ni zaidi ya kalori 180

Hakuna maoni: