Kijana Mohamed Salum ‘Fido’ anayesadikiwa kuwa alikufa
Tukio hilo la aina yake lilitokea Septemba 12, mwaka huu, saa sita mchana wakati shughuli mbalimbali za mazishi yake zikiendelea zikiwa ni pamoja na maandalizi ya chakula cha mchana kwa waombolezaji.
Iko hivi; Fido ni dereva wa bodaboda, kijiwe chake kikiwa Lumumba Mnazi Mmoja, Dar. Inadaiwa kwamba Septemba 10, mwaka huu alikamatwa na polisi wa ‘Tigo’, Lumumba kwa madai ya kutokuwa na kibali cha kuingia mjini, akapelekwa Kituo Kikuu cha Polisi (Central).
Pale kituoni, habari zinadai maafande hawakumruhusu kumpigia simu mkewe ili kumweleza yaliyompata, ndipo ndugu walipoamua kumtafuta kwa siku mbili bila mafanikio.
Waombolezaji wakiwa msibani.
Septemba 11, mwaka huu, mkewe, kaka yake na baba yake mzazi walikwenda Hospitali ya Mwananyamala na kuingizwa chumba cha kuhifadhia maiti (mochwari) ambapo walioneshwa maiti moja! Vilio vikaibuka kwani wote walisema ni Fido. Marehemu huyo aliuawa kwa kugogwa na kitu kizito kichwani na maiti yake ilipelekwa hapo na polisi.
Ndugu hao walitoka na vilio hadi nyumbani na msiba ukawekwa kwa kukusanya mikeka na chakula kuanza kupikwa huku sehemu ya kuzikia makaburini ikitafutwa achilia mbali sanda kupatikana huku ndugu walio mbali wakijulishwa kuhusu msiba huo.
Siku ya tukio, watu wakiwa katika maandalizi ya mwisho kabla ya kuufuata mwili, ndipo Fido alipoibuka na kusababisha tafrani kubwa.Baadhi ya watu waliingia mitini kwa woga huku ndugu wakishangaa iweje maiti itoke mochwari yenyewe? Ndipo Fido alipotangaza kwa sauti kuwa, hakufa, alikuwa polisi.
Kijana Mohamed Salum ‘Fido’ anayesadikiwa kuwa alikufa akila.
“Kweli sijui nisemeje, tuliwataka radhi waombolezaji kwa usumbufu, baadhi walitawanyika kwa wakati huo wengine waliendelea kuwepo hata ndugu zetu wengine wako njiani wakitokea Mbeya na Mtwara.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni