Taifa linaelekea kupata hasara kubwa ya zaidi ya Sh. bilioni 120 baada ya kushindwa kupatikana kwa katiba mpya kama ilivyokusudiwa.
Kiasi hicho cha fedha zitakazopotea bure kinatokana na makadirio ya jumla ya fedha zitakazojumuisha mchakato wote uloiodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, ukianzia wakati wa kuundwa kwa Tume Maalum ya Mabadiliko ya Katiba na pia kuwapo kwa vikao vya Bunge Maalum la Katiba vinavyoendeloea mjini Dodoma na kutarajiwa kusitishwa Oktoba 4 mwaka huu.
Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE na kuwahusisha wachambuzi mbalimbali wa masuala ya siasa na uchumi umebaini kuwa kwa kukadiria, ikiwa wajumbe wote waliopo bungeni hivi sasa watakuwa wakihudhuria kila kikao katika ngwe ya pili iliyoanza Agosti 5, maana yake ni kwamba kila mmoja ataondoka na Sh. milioni 12.9 za posho za siku 43 za kazi pamoja na fedha nyingine kiasi cha Sh. 4,140,000 zitakazotokana na posho watakayoipata katika siku 18 zisizokuwa za kazi.
Inaelezwa kuwa wajumbe hao hulipwa posho ya Sh. 300,000 kila mmoja katika siku za kazi wanazohudhuria kikao huku wanapokosa kikao kwa ruhusa maalum, pamoja na siku zisizokuwa za kazi hupokea posho ya Sh.230,000.
Hadi sasa, wajumbe waliojisajili baada ya kuanza kwa ngwe ya pili wanakadiriwa kuwa 528, idadi ambayo haihusishi wajumbe 101 wakiwamo wanaotoka katika kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao walisusia vikao hivyo tangu April 16, 2014 wakipinga kubadilishwa kwa rasimu iliyowasilishwa na Tume iliyoongozwa na Warioba kutokana maoni yaliyokusanywa kutoka kwa wananchi.
Inaelezwa kuwa kwa hesabu hizo, jumla ya kiasi cha fedha kitakachotumika tangu kuanza tena kwa Bunge hilo Agosti 5 hadi Oktoba 4 kitapanda zaidi kwani hadi kusitishwa kwa bunge hilo katika awamu hii ya pili, kila mmoja atakayehudhuria bila kukosa atapokea jumla ya Sh. 17,040,000.
Hadi kufikia mwishoni mwa wiki iliyopita hakukuwa na takwimu rasmi kutoka ofisi ya Bunge Maalum la Katiba kuhusiana na idadi ya wajumbe waliopo kwenye bunge hilo linaloendelea mjini Dodoma.

Hata hivyo, inakadiriwa kuwa wajumbe wa Bunge hilo waliopo nje ni wabunge 62 kutoka kambi ya Upinzani bungeni, wajumbe 30 wa Chama Cha Wananchi (CUF) wanaotoka katika Baraza la Wawakilishi huku wajumbe wengine wakiwa ni pamoja na wafuasi wa vyama vinavyounda Ukawa vya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NCCR-Mageuzi na pia CUF, walioingia kupitia kundi la wajumbe 201 walioteuliwa na Rais ambao miongoni mwao ni pamoja na Profesa Ibrahim Lipumba, Profesa Abdallah Safari, Julius Mtatiro na Mchungaji Christopher Mtikila wa DP.
Fedha nyingine zilizotumiwa na taifa kugharimia mchakato huo ni Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyotumia Sh. bilioni 67.888 katika kipindi cha takribani mwaka mmoja wa uhai wake, ukarabati jengo la Bunge ukigharimu Sh. bilioni 8.6 na awamu ya kwanza ya Bunge hilo ikitumia Sh. bilioni 27 kwa siku 67; hivyo gharama za jumla kuwa zaidi ya Sh. bilioni 120
TUME YA KATIBA
Iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilitumia takribani Sh. bilioni 69 ambazo Waziri Kivuli katika Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu, aliwahi kueleza bungeni kuwa ni kufuru.
Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2013/14, Bunge liliidhinisha Sh. bilioni 33.944, sawa kiasi kile kile kilichoidhinishwa mwaka wa fedha uliopita.
Fedha hizo zilitumika kulipa posho kwa wajumbe na maofisa wengine wa tume, usafiri, nyumba kwa waliokuwa wanatoka nje ya Dar es Salaam na chakula.
Kadhalika, katika fedha hizo, Serikali pia iliomba Sh. milioni 18 kwa ajili ya kugharamia chakula kwa Wajumbe wa Tume na Sekretarieti watakaopata maambukizi ya ukimwi.
UKARABATI BUNGE
Taarifa zinaeleza kuwa Sh. bilioni 8.6 zilitumika kukarabati ukumbi wa Bunge ili kuweza kuhudumia wajumbe 629 na miundombinu yake na kuweka vifaa vya kisasa vikiwamo vya usalama.
Ukarabati ulihusisha jengo la bunge na miundombinu yake kwa kuweka viti vipya 678 vilivyofungwa kwenye ukumbi huo uliokomba Sh. bilioni 1.6, kurekebisha mfumo wa sauti uliokuwa hausikiki vizuri na kuweka baadhiya vipaza sauti, kuweka vioo visivyopenyeza risasi, paa na Idara ya Kuhifadhi Kumbukumbu za Bunge (hansard).
BUNGE MAALUM
Mei mwaka huu, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, alikaririwa akisema Serikali ilitumia Sh. bilioni 27 kuendesha Bunge Maalum la Katiba kwa siku 67 za awali kabla ya kusitishwa kupisha Bunge la Bajeti.
Bunge hilo ambalo lilirejea tena Agosti 5, kwa siku nyingine 60, inaweza kugharimu zaidi ya Sh. bilioni 20.Hata hivyo, Serikali inaweza kuokoa fedha kidogo baada ya makubaliano kati ya Rais Jakaya Kikwete na Wanachama wa Kituo cha Demokrasia (TCD) wakiwamo wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kuafikiana kuwa sasa Bunge hilo lisitishwe Oktoba 4 badala ya Oktoba 31; kisha Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 itafanyiwa marekebisho ili itumiwe kwenye uchaguzi mkuu wa mwakani.
Makubaliano hayo yamekuwa pigo kwa walalahoi nchini ambao walidhani wangepata Katiba mpya na badala yake Katiba ya sasa itawekwa 'viraka' .

Mbali ya posho, kuna matumizi mengine kama mafuta ya magari, vipuri, karatasi, viburudisho, mawasiliano, umeme wa viyoyozi, maji, karatasi za vyoo, machapisho, kukirimu wageni, kualika wataalamu kutoa ufafanuzi na safari za kikazi, ni wazi kuwa mabilioni yameyeyuka.
HASARA KWA TAIFA
Fedha hizo zaidi ya Sh. bilioni 120 zinazoendelea kupotea kwa kushughulikia katiba ambayo imethibitika kuwa kwa sasa haitapatikana kama ilivyotarajiwa, ni hasara kubwa kwa taifa kwani zingeweza kutumika katika maeneo mengi ya maendeleo.
Kwa mfano, inaelezwa kuwa fedha hizo zingesaidia sana kupunguza tatizo la foleni za magari jijini Dar es Salaam kama zingeelekezwa kwenye mradi wa ujenzi wa barabnara za pembezoni (ring roads).
Katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2013/2014, Wizara ya Ujenzi ilieleza kuwa vipaumbele vyake ni pamoja na kupunguza foleni jijini Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa barabara ya Kigogo – Jangwani (Sh. bilioni 7.6), fidia kwa majengo ya kandoni mwa barabara ya Kigogo-Jangwani (Sh. bilioni 15.8) na kipande cha kilomita tatu cha barabara ya Kimara Korogwe- Kilungule kinachogharimu Sh. bilioni 3.5. Fedha nyingine ni ni Sh. bilioni 13 kwa ajili ya kilomita saba za Mbezi Mwisho-Goba, Sh. bilioni 16 za Tangi Bovu-Goba, Baruti-Msewe (Sh. bilioni 4.6) na Kigogo- Tabata Dampo (Sh. bilioni 5.7). Miradi hii yote ingekamilishwa mara moja kwa mabilion yaliyoelekezwa kwenye mchakato wa kuandika katiba.
Fedha hizo za kugharimia katiba zingetosha pia kujenga zahanati za kisasa 600 ikiwa kila moja itajengwa kwa Sh. milioni 200, kununua madawati 857,000 kwa makaditio ya kila dawati kununuliwa kwa Sh. 140,000 na pia kuchimba visima virefu vya maji 4,800 ikiwa kila kisima kitagharimu Sh. milioni 50.
Aidha, inaelezwa vilevile kuwa fedha hizo (Sh. bilioni 120) zingeweza pia kusaidia ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari na pia kuwapa mikopo wanafunzi 80,000 kwa mwaka wa vyuo vya elimu ya juu ikiwa kila mmoja wao angepatiwa Sh. milioni 1.5.
Kiasi hicho cha fedha zinazoteketea kwa mchakato wa katiba kingeweza pia kuboresha miundombinu ya reli, dawa za binadamu na mifugo na hata shughuli ya usambazaji wa umeme vijijini.
UREFU WA DAR HADI BUKOBA
Katika hatua nyingine, imefahamika kuwa noti milioni 12 za Sh. 10,000 zinahitajika kukamilisha kiasi cha Sh. bilioni 120 na noti hizo zinaweza kupangwa kwa urefu katika barabara itokayo jijini Dar es Salaam hadi Bukoba yenye urefu unaokadiriwa kuwa kilomita 1,379 na bado kiasi kingine kitabaki.
Hesabu hizo zinatokana na ukweli kuwa kwa uchunguzi wa NIPASHE, urefu wa noti moja ya sh. 10,000 ni sawa na sentimita 14.1, hivyo kwa noti milioni 12, umbali wake kwa kuzitandaza ni sawa na sentimita 169,200,000 au kilomita 1692 (kilomita moja ni sawa na sentimita 100,000).

WASOMI WAZUNGUMZA
Mhadhiri mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Semboja Haji, alisema kilichotokea kwenye mchakato wa katiba ni jambo lililotegemewa.
Alisema mfumo wa watu walioteuliwa kuunda Bunge Maalum la Katiba ulidhihirisha kwamba hakuna ambacho kingefanyika zaidi ya kuligharimu taifa.
"Labda niseme tu kwamba siyo hali ambayo sikuitegemea, kwa sababu watu walioteuliwa kwenda kujadili rasimu ya tume hawakuwa na uwezo wa kutuletea kitu cha maana," alisema.
Dk. Semboja alisema pamoja na hali hiyo kudhihirika mapema, anashangaa kwa nini Usalama wa Taifa haukubaini na kumshauri rais jambo la kufanya ili kuepusha hasara na aibu ambayo Taifa imepata kutokana na kuendelea kwa vikao vya Bunge Maalum la Katiba.
Alionya kuwa kama mfumo wa kutumia wanasiasa utaendelea kutumika mwaka 2016, itatuchukua muda mrefu kupata Katiba mpya.
Ikiwa makubaliano ya sasa yatataka mchakato huo uendelee mwaka 2016 baada ya uchaguzi wa mwakani, italazimika kutungwa kwa sheria itakayomtaka rais ajaye atekeleze mchakato huo vinginevyo anaweza kupuuzia.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni