promotion

Jumamosi, 5 Aprili 2014

RICHARD MAVOCAL/ROHO YANGU OFFICIAL VIDEO HD 720.





Rich Mavoko alianza kutoa vipande vya video hii muda mrefu sana kwenye account yake ya instagram lakini baada ya muda wote huo hatimaye ameitoa video nzima.


Story kubwa ya hii video ilikua ni Rich Mavoko kukodisha camera ya gharama kutoka Kenya na kwa ajili ya ku-shoot video hii.





Alhamisi, 27 Machi 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE AONGEA NA WANANCHI WILAYANI MUHEZA, AHITIMISHA ZIARA YA KIKAZI MKOA WA TANGA



































Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mtoto Hassan Mustafa(13) mwenye tatizo la kudumaa muda mfupi baada ya Rais Kikwete kukagua na kuzindua maabara katika shule ya sekondari ya Potwe, wilayani Muheza





MWILI WA MAREHEMU MKUU WA MKOA WA MARA JOHN TUPPA WAWASILI DODOMA LEO



























Askari wakiwa wamebeba mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege Dodoma leo Machi 27, 2014. Marehemu ataagwa kwenye viwanja vya Nyerere Dodoma Machi 28, 2014 kabla ya kusafirishwa  kwenda kilosa kwa mazishi. 
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.



Jumamosi, 8 Machi 2014

MAREHEMU ALIYEKAA MOCHWARI TANGU MWEZI ULIOPITA KUTOKANA NA MGOGORO WA KUMZIKA, HATIMAYE AMEAGWA


























Mama wa marehemu Emmanuel, Hilda Lewi Nambuo Temu akiaga mwili wa                                       mwanaye kwa simanzi.


Ijumaa, 7 Machi 2014

ADHA YA MVUA KUBWA JIJINI DAR ES SALAAM






















Dereva wa Bodaboda, akiwa na abiria wake, wakinyanyua miguu kukwepa kulowa na maji ya mvua yaliyofurika kwenye barabara ya Mbozi, Chang'ombe jijini Dar es Salaam jana. Mvua ya siku mbili tu tayari imeanza kuletakasheshe, si kwa wenye magari pia wenye bodaboda, watembea kwa miguu.

BIBI MJASIRIAMALI WA MAKOPO AENDESHA MAISHA DAR























Makopo yakiwa eneo la nyumba ya bibi huyo ambaye anaonekana kwa mbali akiondoka baada ya kuongea na paparazi wetu.


BASI LA AM COACH LAGONGANA NA LORI HUKO TABORA, TAZAMA PICHA ZA TUKIO HILO


































RIDHIWANI KIKWETE ATOA SIKU 7 KWA WANAOMSHUTUMU KUWA NI BILIONEA WAPELEKE USHAHIDI MAHAKAMANI



































MZUNGU TAPELI ANASWA NA MAHELA KIBAO YA BANDIA HAPA BONGO





















Kamanda Suleiman Kova


































JAN ELOFF AKITOLEWA  NJE YA KITUO CHA POLISI OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM

































JAN ELOFF AKIHOJIWA NDANI YA CHUMBA MAALUM KILICHOPO NDANI YA                                      KITUO CHA POLISI OYSTERBAY

Yule mzungu aliyekuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kutuhuma za kuwatapeli wananchi kwa Euro Feki hatimae amekamtwa akijaribu kununua gari kwa pesa hizo feki. 

Habari za uhakika zilizotua mezani zilisema mzungu huyo ambae ni Raia wa South Africa aliyefahamika kwa jina la  JAN ELOFF ambae anaishi maeneo ya Msasani Jijini Dar.  
Taarifa zilisema mzungu huyo ambae alikuwa anatuhumiwa kumpiga zaidi ya Euro hizo feki 700 mwandishi (jina kapuni) na DTV Bw. Livingstone Mkoi mwanzoni mwa januari mwaka huu kisha kufungua kituo cha polisi Oysterbay nakupatia kumbukumbu hii OB/RB/ 2972/14 KUJIPATIA PESA KWA NJIA YA UDANGANYIFU, pamoja na Kutoa Euro Feki. 
Baada ya tukio hilo la kutapeliwa mwanahabari huyo Jeshi la Polisi lilitangaza msako mkali wa kumtafuta mzungu huyo ambae alikuwa akishirikiana na wadada wawili ambao ni raia wa Cameroon na Nigeria pamoja na mwanaume wa kitanzania ambao baada ya tukio la kukamatwa mwenzao wanaendelea kutafutwa usiku na mchana na tayari ameshawataja wenzake anaoshirikiana nao.Kufuatia kukamtwa kwa mzungu huyo wananchi wengi wamempongeza Kamanda Kova kwa kufanikisha kukamatwa mzungu huyo.  
Hata hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni limetoa rai kwa mtu yeyote ambae amewahi 'kupigwa' na mzungu huyo basi wafike haraka kituo cha polisi Oysterbay kwa ajili ya kumtambua mzungu huyo.


Jumatano, 5 Machi 2014

Picha/Video: Chatu mwenye futi 10 alivyommeza mamba mzima mzima, walipigana kwa saa 5


























RAIS KIKWETE ATEMBELEA VIKOSI VYA JWTZ VYA KOMANDO NA UHANDISI MEDANI MKOANI MOROGORO


Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Kikosi cha Komando kuanza ziara yake ya kujionea hali na utimamu wa vikosi vya JWTZ Mkoani Morogoro.

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Rais Jakaya Kikwete amefanya Ziara ya siku moja katika Vikosi vya Jeshi la Wanannchi wa Tanzania (JWTZ) vya Komando na Uhandisi Medali vilivyopo Mkoani Morogoro.

Akizungumza katika kikao maalum na Maafisa Askari wa vikosi hivyo,Rais Kikwete amesema ameridhishwa sana na utimamu wa vikosi hivyo kimafunzo na pia amehidi kukiongezea vifaa zaidi kikosi cha Uhandisi wa Medani ili kiweze kupambana na majanga hapa nchini.

Rais Kikwete pia amelitaka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kubuni mikakati ya kuondokana na Makazi ya muda. 
Katika Kikao hicho,Rais Kikwete aliligusia swala ta tatizo la Maji linalovikabili vikosi hivyo,ambapo ameahidi kulishungulikia ndani ya kipindi hiki cha mwaka 2014.


Katika ziara hiyo,Rais aliambatana pia na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi Makao Makuu ya Jeshi, Makamishna Wizarani na Wajumbe wa Mabaraza ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya na Mkoa wa Morogoro.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akivuka juu ya daraja jipya la medani lililojengwa kumuonesha uwezo wa Wahandisi Medani wa JWTZ kuendelea kusaidia usafirishaji wa zana na vifaa hata pale madaraja ya kudumu yanapoharibiwa kwa namna yoyote ile. 
Picha/habari na Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na JKT



























Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa maelezo kwa kutumia mchoro kuonesha mzunguko mzima wa maeneo atakayotembelea katika kikosi cha Komando.

Magazeti ya leo March 05 2014